Zaidi ya mabomu 9000 yameteguliwa Iraq na Syria

Shirika la The Mines Advisory Group, linasema limetegua mabomu zaidi ya 9,000 katika miezi sita iliyopita Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shirika la The Mines Advisory Group, linasema limetegua mabomu zaidi ya 9,000 katika miezi sita iliyopita

Shirika linalopinga matumizi ya mabomu yanatotegwa ardhini, limesema kuwa fedha zaidi zinahitajika kupambana na tatizo linalozidi nchini Syria na Iraq.

Shirika hilo, The Mines Advisory Group, linasema limetegua mabomu zaidi ya 9,000 katika miezi sita iliyopita, katika maeneo ambayo yalikuwa yamedhibitiwa na Islamic State.

Linasema zinahitajika dola milioni 100 zaidi, kutegua mabomu yaliyotegwa karibuni, na maelfu mengine yaliyobaki kutoka na vita vya zamani.

Wito huo wa mchango, umetolewa ikiwa imetimia miaka 20 kamili, tangu Hayati Princess Diana kuzuru maeneo yaliyozikwa mabomu huko Angola ziara iliyosaidia kuzindua ulimwengu kuhusu tatizo hilo.