Iran: Mkataba wa nuklia hautajadiliwa tena

Iran iliafikia mkataba wa nuklia na mataifa makubwa duniani Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iran iliafikia mkataba wa nuklia na mataifa makubwa duniani

Mpatanishi mkuu wa mpango wa nukilia wa Iran na mataiafa makubwa duniani, amesema kuwa mapatano yaliyoafikiwa hayatajadiliwa tena wakati rais mteule wa Marekani anajiandaa kuingia madarakani.

Abbas Araghchi ambqye pia ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Iran, alirejelea matamshi ya onyo kutoka kwa kiongozi mkuu nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambapo alisema kuwa watachoma mkataba huo ikiwa utavurugwa.

Trump ametaja makubaliano hayo ya kupunguza shughuli za kinyukila za Iran uliofakiwa mwaka mmoja uliopita kama mabaya zaidi kuwai kuafikiwa.