Waasi wa M23 waingia DRC

Waasi wa M23 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wa M23

Utawala nchini Jamhuri ya Demokarsi ya Congo unasema kuwa karibu watu 200 waliokuwa wanachama wa kundi la waasi wa M23 wameingia nchini mwake kutoka nchi jirani ya Uganda.

Msemaji wa serikali Lambert Mende, amesema kuwa jeshi la Congo limekabiliana na watu hao.

Ameilaumu Uganda kwa kuwaruhusu watu hao kuvuka mpaka. Waasi wa M23 ni kutoka kundi la Tutsi ambalo lilishindwa na jeshi la Congo mwaka 2013.

Serikali ya DRC kisha ikaendesha harakati za kuwapokonya silaha lakini baadaye harakati hizo zikasitishwa.

Waasi hao wa zamani kwa sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi nchini Uganda na Rwanda.

Image caption Waasi hao wa zamani kwa sasa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi nchini Uganda na Rwanda.