Serbia yaionya vikali Kosovo

Kosovo ilitangaza uhuru wake kutoka Serbia mwaka 2008
Image caption Kosovo ilitangaza uhuru wake kutoka Serbia mwaka 2008

Rais wa Serbia Tomislav Nikolic ameionya Kosovo kuwa nchi yake italinda kila eneo la mpaka wake na ikiwezekana itatuma jeshi kwenda kulinda raia wa Serbia wanaoshi nchini Kosovo.

Hii inajiri baada ya kuibuka msukosuko kati ya majirani hao wa Balkan. Siku ya Jumamosi Serbia ilijaribu kutuma treni kwenda eneo lenye Waserbia nchini Kosovo, lakini ikasimama kabla haijafika kwa mpaka.

Kosovo inasema kuwa itachukua kila hatua kuizuia treni hiyo ambayo ilikuwa na mapambo yayoashiria kuwa Kosovo ni Serbia.

Bwana Nikolic aliilaumu Kosovo wa kutafuta mzozo.

Kosovo ilitangaza uhuru wake kutoka Serbia mwaka 2008, lakini Serbia ikiungwa mkono Urusi huitambua hatua hii.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Treni hiyo ilikuwa na mapambo yayoashiria kuwa Kosovo ni Serbia