Wafungwa 30 wafariki katika machafuko Brazil

Baadhi ya wafungwa walitoroka kupitia paa la gereza wakati wa fujo hizo
Image caption Baadhi ya wafungwa walitoroka kupitia paa la gereza wakati wa fujo hizo

Taarifa za kutisha zimeanza kujitokeza nchini Brazil kutokana na machafuko yaliyotokea usiku kucha katika jela la Alcaçuz baada ya kuibuka kwa mgomo.

Mamlaka nchini Brazil zinasema takriban wafungwa thelathini waliuawa na wafungwa wenzao, wataalamu wakuchunguza masuala ya mauwaji wamesema walioathirika zaidi walikuwa wamekatwakatwa au kutolewa baadhi ya viongo.

Mgomo huo ulianza jumamosi mchana, wanakikundi wa kikundi cha wahalifu waliopo katika magereza ya Brazil na kushambulia kundi hasimu lenye msimamo tofauti.

Hii ni mara ya tatu kwa mgomo mkubwa kama huu kujitokeza kwa wafungwa nchini Brazil mwezi huu, mamia ya wafungwa wamefariki gerezani katika miji ya Amazonas na Roraima.