Serbia kutuma jeshi kuwalinda raia wake Kosovo

Treni ya Serbia iliyokuwa imeandikwa maandishi maalum kwa ajili ya raia wake
Image caption Treni ya Serbia iliyokuwa imeandikwa maandishi maalum kwa ajili ya raia wake

Rais wa Serbia Tomislav Nikolic ameionya Kosovo kwa kuwataarifu kwamba, akiona umuhimu nchi yake itatuma majeshi ili kuwalinda wananchi wa Serbia wanaoishi nchini Cosovo.

Siku ya Jumamosi Serbia ilitaka kutuma Treni yenye maandishi yakiwa na ujumbe unaodai kuwa Kosovo ilikuwa ni sehemu ya eneo la nchi ya Serbia, kuelekea katika eneo la asili nchini Serbia kaskazini mwa Kosovo lakini ilisimama kabla ya kufika mpakani.

Serikali mjini Pristina imesema itachukua taadhari madhubuti kuzuia treni hiyo

Bwana Nikolic ameituhumu Kosovo kwa kutafuta ugomvi.

Mwandishi wa habari wa BBC ametaarifu kuwa uchaguzi wa urais nchini Serbia unaotarajiwa kufanyika mwezi April kuna uwezekano zaidi wa kuwepo kwa ishara za kukata rufaa kwa kura za utaifa.

Nchi ya Kosovo ilipata uhuru kutoka kwa Serbia mwaka 2008 lakini Serbia pamoja na Urusi hawalitambui hili.