Chuo kimoja kikuu chashambuliwa kwa bomu Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mhanga mmoja alizuiwa na walinda usalama katika lango la Chuo hicho

Raia wawili na walipuaji wawili wa kujitoa kufa, wamefariki katika shambulio la bomu kwenye Chuo Kimoja kikuu nchini Nigeria.

Milipuko hiyo miwili ya kujitoa mhanga iligonga Chuo Kikuu cha Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Yamkini watu wanne wameuwawa, wakiwemo walipuaji hao wa kujitolea kufa.

Msemaji wa polisi ameiambia BBC kuwa, walimkabili mmojawepo wa washambuliaji hao - msichana wa umri wa miaka 12 hivi, katika lango la Chuo hicho.

Huku akishukiwa kubeba bomu, walimpiga risasi, na hapo ndipo bomu alilokuwa amejifunga likalipuka.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mlipuaji mwingine alijilipua akiwa ndani ya msikiti

Dakika chache baadaye kulitokea mlipuko mwingine wa bomu katika msikiti mmoja uliokuwepo karibu na lango kuu la Chuo hicho.

Watu 15 wameripotiwa kujeruhiwa

Kwa muda mrefu mbinu za kutumia milipuko ya mabomu ya kujitoa mhanga yamekuwa yakitumika na kundi la Boko Haram, mara nyingi wakiwatumia wasichana wadogo.

Huku serikali ya Nigeria ikidai kuwafurusha wanamgambo wa Boko Haram kutoka katika makao yao waliokuwa wakiyadhibiti, inaonekana kuwa wapiganaji hao wa kiislamu wangali bado wanaweza kushambulia.

Kumekuwepo ongezeko la mashambulio ya aina hii, inayopenya hadi mmji mkuu wa Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.