Kesi ya Ongwen yaanza tena ICC

Dominic Ongwen ndiye kamanda wa kwanza wa LRA kufikishwa ICC Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dominic Ongwen ndiye kamanda wa kwanza wa LRA kufikishwa ICC

Kesi ya kamanda wa kwanza kabisa wa kundi la waasi nchini Uganda la Lord's Resistance Army (LRA), kuwahi kufikikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita imeanza tena.

Dominic Ongwen anakabiliwa na mashtaka 70 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na utumwa.

Alifikishwa mbele ya mahakama hiyo tarehe 6 mwezi Disemba ambapo alikana mashtaka hayo.

Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda, aliiambia mahakama kuwa ushahidi unamuonyesha kama muuaji na pia mbakaji.

Ndiye mtoto wa zamani wa kwanza mwanajeshi kufikishwa mbele ya mahakama ya mjini Hague.

Bwana Ongwen alikuwa kijana mdogo wakati alitekwa nyara na kuingizwa kwa kundi la LRA.

Image caption Bwana Ongwen alikuwa kijana mdogo wakati alitekwa nyara na kuingizwa kwa kundi la LRA.