El-Adde: Madhila ya familia zilizowapoteza jamaa Kenya
Huwezi kusikiliza tena

El-Adde: Madhila ya familia zilizowapoteza jamaa Kenya

Ni mwaka mmoja tangu kundi la wanamgambo wa Al shabaab nchini Somalia lilipovamia kambi ya wanajeshi wa Kenya ya El Adde iliyoko nchini humo.

Ingawa bado serikali ya Kenya haijatangaza idadi rasmi ya maafisa waliofariki, mauaji hayo yamebadili maisha ya familia nyingi zilizokuwa zinawategemea maafisa hao kuwa yenye uchungu mwingi.

Kwa sasa familia hizo zinatoa wito kwa majeshi ya AMISOM na serikali ya Kenya ili kuwawezesha kuendelea na maisha yao.

Abdinoor Aden amezuru mji wa Narok, eneo la bonde la ufa nchini humo na kuzungumza na Rose Serea Koronoi, mmoja wa wajane wa maafisa hao.

Mada zinazohusiana