Rolls Royce watoa mchanganuo wa mapato yao yaliyodaiwa kuwa hongo

Mwezi wa pili itatoa mchanganuo kamili
Image caption Mwezi wa pili itatoa mchanganuo kamili

Watengenezaji wa injini Rolls Royce wamesema wamefikisha dola milioni 800 za gharama za makaazi kwa mamlaka za Uingereza, Marekani na Brazili ambapo fedha hizo zinafananishwa na hongo pamoja na ubadhilifu.

Kampuni ya Uingereza inayotengeza injini za ndege, meli pamoja na vyombo vya ulinzi vya majini, wamesema makubaliano yaliyofanywa na waamuzi kuhusu makosa hayo katika masoko ya nje ikiwemo Indonesia pamoja na China.

Imesema ilitoa taarifa kwa mamlaka husika nchini Uingereza kuhusiana na tatizo hili mwaka 2012 na itaendelea kutoa ushirikiano wakutosha.

Kampuni ya Rolls -Royce itatoa mchanganuo wa taarifa za mwaka mzima ifikapo mwezi wa pili mwaka huu, na kutoa taarifa katika masoko husika katika mabadiliko ya makaazi.