Muuaji wa watu 39 kwenye klabu ya Reina Istanbul akamatwa

Picha za muuaji huyo zilisambazwa na polisi baada ya kufanya shambulizi hilo
Image caption Picha za muuaji huyo zilisambazwa na polisi baada ya kufanya shambulizi hilo

Vyombo vya habari nchini Uturuki vimesema mshukiwa mkuu katika shambulizi la mkesha wa mwaka mpya mjini Istanbul amekamatwa.

Abdulkadir Masharipov anaaminika kufanya shambulizi hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu 39 kwenye klabu ya usiku ya Reina.

Image caption Abdulkadir baada ya kukamatwa

Amekamatwa katika mtaa wa Esenyurt mjini Istanbul.

Raia wa Israel, Ufaransa, Tunisia, Lebanon, India, Ubelgiji, Jordan na Saudi Arabia walikuwa miongoni mwa waliouawa huku mamia ya watu wakijeruhiwa.