Mwanamke mwenye macho ya kushangaza kuanza maisha mapya Afghanistan

Sharbat Gula kando na picha yake aliyopigwa akiwa mtoto mkimbizi Haki miliki ya picha BBC / Steve McCurry
Image caption Sharbat Gula kando na picha yake aliyopigwa akiwa mtoto mkimbizi

Mwanamke raia wa Afghanistan ambaye alipata umaarufu kutokana na picha yake ya mwaka 1985, amezungumza na BBC kuhusu matumaini yake ya kuanza maisha upya, baada ya kufukuzwa kutoka nchini Pakistan.

Sharbat Gula kwa sasa anaishi na mwanawe wa kiume wa umri wa miaka mitano na binti zake watatu mjini Kabul, ambapo anasema kuwa anataka kuishi miasha ya kawaida baada ya miaka kadha ya hali ngumu .

Picha yake akiwa na umri wa miaka 10, ilipata umaarufu kuhusu wakimbizi wa Afghanistan wanaokimbia vita.

Kama raia wengine wa Afghansitan Sharbat Gula, alitafuta hifadhi nchini Pakistan na kuishi huko kwa miaka 35, lakini alikamatwa na kutimuliwa nchin humo mwaka uliopita kwa kupata vitambulisho vya Pakistan kinyume cha sheria.

"Tulikiwa na maisha mazuri huko, tulikuwa na majirani wazuri, tuliishi na ndugu zetu Wapashtun. Lakini sikutarajia kuwa serikali ya Pakistan ingenitendea haya."aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sharbat Gula alihukumiwa kifungo cha siku 15 jela

Akiwa na na umri wa miaka ya 40 na mgojwa, Sharbat Gula bado macho yake ni kutia hofu.

Anasema kuwa alikuwa tayari ameuza nyumba yake nchini Pakistaa, kwa sababu alihofia kuwa angekamatwa kwa kutokuwa na stakabadhi halali.

Siku mbili baadaye kabla ya kupanga kuondoka na kurudi Afghanistan, nyumba yake ilivamiwa ambapo alikamatwa na kupelekwa gerezani.

Pakistna imetoa amri ikiwataka wakimbizi wote milioni mbili wa Afghanistan waondoke nchini mwake,

Sharbat Gula anaamini kuwa utawala ulitaka kumkamata kabla hajaondoka.

Haki miliki ya picha REUTERS/Mohammad Ismail
Image caption Sharbat Gula kwa sasa amerudi Afghanistan ambapo serikali imeahidi kumununulia nyumba

Alitumikia kifungo cha siku 15 , wiki ya kwana gerezani na ya pili hospitalini ambapo alitibiwa ugonjwa wa hepatitis C.

Baada ya Pakistan kutambua kuwa itajichafulia jina, ilimuomba aendelee kuishi lakini akakataa.

Mumewe na bintiye wote walifariki nchini Pakistan na wamezikwa Peshawar

Makaribisho mema

Sharbat Gula alikutana na rais wa Afghanistan Ashraf Ghani katika ikulu ya rais aliporudi na baadaye kukutana na rais wa zamani Hamid Karzai.

"Walinionyesha heshima, wakanipa makaribisho mema, ninawashukuru, Mungu awatendee mema."

Serikali imeahidi kuisaidia kifedha familia yake na kumununulia nyumba mjini Kabul.

"Nina matumaini serikali itatimiza ahadi zake," aliiambia BBC.

Haki miliki ya picha REUTERS/Mohammad Ismail
Image caption Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani alimkaribisha ikulu