Wanaume wasio na kura kunyimwa tendo la ndoa Kenya

Baadhi ya wanaume wakisajiliwa kama wapiga kura nchini Kenya kufuatia kuanzishwa kwa shughuli hiyo siku ya Jumatatu
Image caption Baadhi ya wanaume wakisajiliwa kama wapiga kura nchini Kenya kufuatia kuanzishwa kwa shughuli hiyo siku ya Jumatatu

Mbunge mmoja ametoa wito kwa wanawake waliopo katika maeneo yenye wafuasi wengi wa upinzani nchini Kenya kutofanya mapenzi na waume zao ambao hawajajisajili kama wapiga kura.

Kulingana na gazeti la The Standard nchini humo, mwakilishi wa wanawake mjini Mombasa Mishi Mboko amewataka wanawake nchini humo kuwanyima wanaume zao haki zao za kindoa ili kuwashinikiza waende kujisajili kama wapiga kura ilinkujiandaa kwa uchaguzi wa mkuu ujo unaofanyika tarehe 8 mwezi Agosti.

Akizungumza katika uwanja wa maonyesho ya kilimo katika eneo la Mkomani Bi Mboko alisema kuwa ngono ni kifaa kizuri kinachoweza kuwashinikiza wanaume kukimbilia kujisajili katika shughuli hiyo ilionza siku ya Jumatatu.

Kulingana na gazeti hilo hatahivyo, mumewe Mboko hatonyimwa haki hiyo ya ndoa kwa uwa tayari amejisajili kama mpiga kura.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwakilishi wa wanawake mjini Mombasa Mishi Mboko

''Wanawake huu ndio mpango munaofaa kuutumia.Ni mpango muziri sana.Wanyimeni haki yao ya kufanya mapenzi hadi pale watakapowaonyesha cheti cha kupiga kura'', alisema.

Mboko aliongezea kwamba imefikia wakati ambapo wanawake wanafaa kutumia ngono kuwalazimisha waume zao kuchukulia shughuli ya usajili wa wapiga kura na umuhimu mkubwa.