Mke wa muuaji wa watu 49 Florida ahukumiwa kwa kumsaidia mumewe

Mwanaume huyo aliuwawa kwa risasi na polisi katika ukumbi huo.
Image caption Mwanaume huyo aliuwawa kwa risasi na polisi katika ukumbi huo.

Mjane wa mwanaume aliyeuwa watu 49 kwa kushambulia kwa bastola watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja waliokuwa katika ukumbi wa starehe katika mji wa Florida huko nchini Marekani, amehukumiwa kwa kumsaidia mumewe katika kuvunja sheria.

Akisomewa mashtaka kwa mara ya kwanza katika mahakama katika jimbo la California Noor Salman hakukata rufaa.

Mwanamke huyo atatumikia kifungo jela kama akikutwa na hatia.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa mwanamke huyo alikuwa akifahamu kuwa mumewe alikwa akipanga shambulio katika ukumbi huo wa starehe maarufu kama Pulse nightclub.

Mwanaume huyo alikiri kuwa na mahusiano na kundi la wapiganaji wa kiislamu (IS)