Trump atuhumiwa kwa uongo

Summer Zervos ni miongoni mwa wanawake waliolalamikia kunyanyaswa kijinsia na Trump
Image caption Summer Zervos ni miongoni mwa wanawake waliolalamikia kunyanyaswa kijinsia na Trump

Mwanamke aliyemtuhumu Rais mteule wa marekani Donald Trump kwa unyanyasaji wa kijinsia, anamtuhumu kwa kosa la kashfa kwasababu Trump alikanusha madai haya na kusema kuwa ni ya uongo.

Summer Zervos alikuwa ni mmoja kati ya wanawake waliotoa madai kumhusu Donald Trump wakati wa kampeni za Urais nchini Marekani ambapo Trump alikanusha madai hayo.

Madai hayo yanaonyesha kwamba Rais Mteule wa Marekani Donald Trump alimkashifu na kumkebehi mwanamke huyo, aliyekuwa mgombea katika kipindi cha Televisheni cha Bwana Trump aliyeigiza kama mwanafunzi, na kumrushia maneno ya uongo.

Mwanasheria wa mwanamke huyo alipitisha jaribio la kubaini Uongo.