Ndege yazindua viti vya wanawake pekee India

Kampuni ya ndege ya Air India imetenga viti vya wanawake pekee katika ndege zake
Image caption Kampuni ya ndege ya Air India imetenga viti vya wanawake pekee katika ndege zake

Kampuni ya ndege ya Air India hii leo inazindua ndege itakayokuwa na viti vya wanawake pekee kwa lengo la kukabiliana na unyanyasaji wa kingono .

Viti sita vitahifadhiwa wanawake, kwa ndege kadhaa.

Wanawake kadhaa akiwemo muhudumu mmoja wa ndege wamelalamikia ndege hiyo wakidai kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kingono na abiria wa kiume.

Viti maalum vya wanawake katika ndege

Mkuu wa muungano wa Abiria nchini humo amepinga mpango huo wa viti, akiutaja kuwa wa kiubaguzi.

Hatua ya kutenge viti kulingana na jinsia fulani sio jambo la kawaida kimataifa.