Aliyekuwa rais wa Marekani George Bush alazwa

Aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush alazwa hospitalini
Image caption Aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush alazwa hospitalini

Vyombo vya habari nchini Marekani vimesema kuwa aliyekuwa rais wa taifa hilo George Bush anapata matibabu katika hispitali moja ya Houston katika jimbo la texas.

Maelezo kuhusu hali yake hayajatolewa ,lakini mkuu wa wafanyikazi wake amenukuliwa akisema kuwa bw Bush aliye na umri wa miaka 92 yuko katika hali nzuri na kwamba huenda akatolewa na kwenda nyumbani katika siku chache zijazo.

Bush kama marais wengine wa zamani anatarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Donald Trump katika sherehe itakayofanyika siku ya Ijumaa.