Je, Afrika itamkumbuka vipi rais Obama ?

Obama alizuru Afrika zaidi ya marais wote wa Marekani waliokuwepo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Obama alizuru Afrika zaidi ya marais wote wa Marekani waliokuwepo

Kuchaguliwa kwa rais Barrack Obama kama rais wa kwanza mweusi kulichangia pakubwa wengi kupatwa na dhana kwamba bara la Afrika litanuifaka sana na sera za kigeni za Marekani.

Mafanikio ya uongozi wake kwa wengi hayajitimiza waliyotarajia.

Hata hivyo utawala wake umefanya mapinduzi katika sera za uhusiano wa Afrika na Marekani kutoka kwa utoaji wa misaada na kuangazia biashara.

Mwandishi wa BBC Nancy Kacungira anaangazia utawala wa Obama Marekani kwa Afrika

Image caption Yegonizer, msanii wa kuchora asema watu hupendelea sana picha za rais Obama

Studio moja ya uchoraji iliopo katika mji mkuu wa Nairobi inaonyesha ishara za umuhimu wa rais Obama uliotia fora barani Afrika wakati alipokuwa rais wa taifa lenye uwezo mkubwa duniani.

Yegonizer, Mchoraji anasema picha zake za Obama zimeuza sana, kwa jumla amependwa na watu wengi kwa hivyo wengi wanaoingia hupendelea michoro yake.

Obama alizuru mataifa manne Afrika katika ujio wake wanne barani Afrika, ikilinganishwa na marais wote wa awali wa Marekani

Utawala wa Obama ulianzisha kambi za kijeshi katika mataifa zaidi ya kumi Afrika.

Lakini wakati ambapo Marekani iliingilia kati siasa za Libya, ni hatua ambayo ilivutia wengi hadi wakosoaji.

Obama mwenyewe alikiri kwamba alijuta sana hatua ya kutekeleza sera zake za kigeni dhidi ya Libya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uongozi wa rais Obama huenda sio vile ulivyotarajiwa na wengi barani Afrika lakini mfano wake bado ni thabiti

Obama aliamini kwamba Afrika ilihitaji biashara, na si misaada, swala ambalo aligusia katika mohojiano yake na BBC mwaka 2015

Dola bilioni nane za misaada ambazo Marekani ilitumia barani Afrika ni asilimia ndogo sana ukilinganisha na nchi zingine.

Afghanistan na Israeli hupokea misaada zaidi kushinda mataifa 42 kwa pamoja kusini mwa jangwa la sahara.

Afghanistan inapokea bilioni 5.5 na Israeli nayo ikipokea dola bilioni tatu nukta moja

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Katika moja ya ziara zake barani Afrika, Obama alisema kwamba mabadiliko yataletwa na vijana

Katika mwaka 2013, Obama alianzisha mradi wa Power Africa wa kusambaza umeme mara dufu barani Afrika, mpango ambao hatma yake haijulikani, baada rais mteule Donald Trump kuupinga vikali ulipozinduliwa

Katika moja ya ziara zake barani Afrika, Obama alisema kwamba mabadiliko yataletwa na vijana, na uhusiano wake na vijana barani utasalia katika nyoyo za wengi

Mradi wa Young African Leaders uliozindulia mwaka 2010 umesababisha watu 250,000 kuungana nao.

Image caption Mjasiriamali Eric Muthomi aliimarisha biashara yake baada ya mafunzo

Mjasiriamali Mkenya Eric Muthomi ni mmoja wao

"Tumechangisha zaidi ya dola elfu mia moja kutokana na mradi wa YALI tumeeza kuona maendeleo kwa biashara mara kumi zaidi kutoka mradi wa YALI uanzishwe mwaka wa elfu mbili na kumi na nne"

Ujasiriamali, biashara na uwekezaji ni mipango ambayo ilipewa kipaombele na rais Obama katika jitihada zake za kutekeleza sera za ushirikiano wa Marekani na Afrika

Kwa Afrika, utawala wa Obama na athari zake kwa njia nyingi hazijulikani.

Utawala utakaomrithi utaamua ni sera zipi zitakazoendela na zipi zitakazotupiliwa mbali.