Baada ya kimya cha muda mrefu,msanii Ditto arejea kwa kishindo katika ulimwengu wa muziki nchini Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Ditto arejea kwa kishindo katika anga za muziki,Tanzania

Waswahili wanasema kimya kingi kina mshindo, na bila shaka ukiona Kobe kainama jua anatunga sheria. Misemo hii ni michache katika mingi ambayo Lameck Ditto maarufu Ditto amerejea baada ya kukaa

kimya kwa takribani miaka mitano na baadaye kurejea katika Tasnia ya muziki na wimbo unaotajwa kuwa moja ya tungo zinayopendwa zaidi kwa sasa nchini Tanzania.

Ili kuupata undani wa wimbo huu uliopewa jina 'Moyo sukuma damu',Mwandishi wa BBC Arnold Kayanda anazungumza na mwanamuziki huyo.