Adama Barrow kuapishwa Senegal huku Jammeh akikatalia madaraka

Adama Barrow amekuwa nchini Senegal tangu Jumapili Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Adama Barrow amekuwa nchini Senegal tangu Jumapili

Mtu ambaye alishinda uchaguzi unaokumbwa na utata nchini Gambia anasema kwa ataapishwa kama rais wa anchi kwenye ubalozi wa Gambia ulio kwenye nchi jirani ya Senegal

Ujumbe ulioandikwa kwenye akaunti za Adama Barrow za mitandao ya kijamii uliiwaalika watu kuhudhuria sherehe hiyo.

Jitihada za mwisho za viongozi wa kanda za kumshawisha Yahya Jammeh kuondoka madarakani kama rais zimeshindwa.

Alishindwa uchaguzi mwezi uliopita lakini anataka matokeo hayo kufutwa akidai kuwepo itilafu.

Vikosi vya wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi viko tayari kushinikiza mabadiliko ya mamlaka nchini Gambia, nchi ambayo ni maarufu kwa watalii.

Vikosi vya Senegal vimesalia kwenye mpaka na Gambia huku muda wa mwisho wa bwana Jammeh kuondoka madarakani ukikamilika usiku wa manane.

Hatua za kijeshi zinaungwa mkono na Nigeria pamjaa na nchi zingine za kanda.

Bwana Barrow amekuwa nchini Senegal tangu Jumapili baada ya mwaliko kutoka kwa viongozi wa nchi za Afrika, wanaounga mkono ushidi wake.

Rais mteule aliandika katika mtandao wa Twitter na Facebook akisema kuwa ataapishwa mwendo wa saa 16:00 GMT (saa moja Afrika Mashariki) kwenye ubalozi wa Gambia mjini Dakar, Senegal.

Takriban watu 26,000 nchini Gambia, walio na hofu kuwa kutazuka ghasia, wamekimbilia usalama nchini Senegal.

Nao watalii kutoka Uingezrea na Uholanzi wanazidi kuondolewa kutoka taifa hilola magharibi mwa Afrika.

Image caption Gambia