Makamu wa rais wa Gambia ajiuzulu

Makamu wa rais wa Gambia Isatou Njie-Saidy Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makamu wa rais wa Gambia Isatou Njie-Saidy

Makamu wa rais nchini Gambia Isatou Njie-Saidy amejiuzulu saa chache kabla ya muda wake wa kuongoza kutimia ,AFP imenukuu duru za familia yake.

Waziri wa mazingiura na elimu ya juu pia alijiuzulu,ikiwa ni msururu wa mawazuri kumtoroka bw Jammeh kufuatia hatua yake ya kukataa kujiuzulu baada ya zaidi ya miongo miwili afisini AfP imeripoti.

Wakati huohuo wakili wa rais Yahya Jammeh ametorokea nchini Senegal baada ya kumuandikia barua rais Jammeh akimtaka kuachilia mamlaka gazeti la Nigeria Primium times limesema.

Edu Gomez alisema kuwa amemfanyia kazi Jammeh chini ya shinikizo chungu nzima .

Haki miliki ya picha Twittter
Image caption Barua ya wakili wa Yaya Jammeh baada ya kutorokea Senegal

Gazeti hilo pia limenukuu barua hiyo ikisema: Siku ya Jumanne tarehe 17 mwezi Januari 2017, mwanangu na mimi tulifanya uamuzi muhimu kutafuta hifadhi katika taifa jirani la Senegal.Hatua hii tuliona ni muhimu kutokana hofu inayoendelea kutanda na wasiwasi kila wakati.

BBC hatahivyo haijapata uthibitisho huru wa ripoti hiyo.

Bw Gomez alimwakilisha Jammeh katika harakati za kufutilia mbali ushindi wa kiongozi wa upinzani Adama Barrow katika uchaguzi wa tarehe mosi Disemba.