Jaji wa mahakama kuu afariki kwenye ajali Brazil

Teori Zavascki alikuwa akisubiria kutoa hukumu kwa kesi ya kampuni ya Petrobras
Image caption Teori Zavascki alikuwa akisubiria kutoa hukumu kwa kesi ya kampuni ya Petrobras

Aliyekuwa jaji katika mahakama kuu nchini Brazili Teori Zavascki amefariki katika ajali ya ndege.

Ndege hiyo ndogo aliyokuwa akisafiria ilianguka baharini katika pwani ya mji wa Rio de Janeiro.

Jaji huyu alikuwa akisimamia uchunguzi wa kesi ya rushwa katika kampuni kubwa ya ujenzi ya serikali inayoitwa Petrobras.

Alitakiwa kuamua kama atakubali ushahidi uliotolewa na mashuhuda kuhusu watendaji 80 wa kampuni hiyo kubwa ya ujenzi (Odebrecht) iliyoko huko Amerika ya Kusini.

Kampuni hiyo imekubali kulipa mabilioni ya dola kama rushwa ili kushinda mikataba duniani kote.

Inadhaniwa kuwa huenda baadhi ya shahidi zilikuwa zinawahusu baadhi ya viongozi wakubwa wa kisiasa akiwemo Rais wa Brazil Michel Temer.