Barack Obama atoa msamaha kwa wafungwa

Marekani
Image caption Barack Obama

Katika siku yake ya mwisho madarakani, Rais Barack Obama amebatilisha vifungo vya wafungwa mia tatu na thelathini, wahalifu wengi wao wakiwa wa dawa za kulevya.

Mshauri wa Ikulu ya Marekani, Neil Eggleston, amesema kwamba mtazamo wa rais Obama ni kwamba kila mtu anahitaji kupewa nafasi nyingine ya kurekebisha maisha na makosa yake.

Alisema ni idadi kubwa ya msamaha kwa wafungwa kuwahi kutolewa kwa siku moja.katika kipindi cha miaka nane ya uongozi wake, amefanikiwa kupunguza vifungo vya wafungwa elfu moja mia saba na kumi na watano kuwahi kutolewa na watangulizi wake nchini Marekani.