Carter: Shambulizi la Libya limeua washukiwa wanane

Carter amesema wengi wa waliouawa waliwahi kufanya matukio ya kihalifu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Carter amesema wengi wa waliouawa waliwahi kufanya matukio ya kihalifu

Waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton Carter, amesema shambulizi la anga lililowalenga wapiganaji wa kiislamu nchini Libya limeuwa zaidi ya washukiwa wanane.

Shambulizi hilo lilitekelezwa na mpiga shaba wa umbali mrefu wa Marekani likielekezwa katika vikundi viwili vya wapiganaji wa kiislamu siku ya Jumatano, katika eneo la jangwa Kusini Magharibi mwa Pwani ya Mji wa Sirte.

Bwana Carter amesema wengi wa waliofariki inaaminika kuwa walikuwa washambuliaji wa mara kwa mara huko Ulaya.

Maafisa wamearifu kuwa shambulizi hilo la anga, lilitekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Libya chini ya Mkataba wa Kitaifa wa Tripoli.