Marekani: Nani watatumbuiza wakati wa kuapishwa kwa Donald Trump?

3 Doors Down Haki miliki ya picha AFP

Wanamuziki wengi nyota walikataa kutumbuiza sherehe ya kuapishwa kwa Donald Trump.

Wengi walikuwa wanamuunga mkono mpinzani wa Trump, Hillary Clinton, na hawakufurahishwa na sera za mwanachama huyo wa Republican hasa kuhusu wanawake, wahamiaji na dini.

Lakini bado Bw Trump amewapata wanamuziki nyota wa kutumbuiza siku hii yake muhimu.

Hata hivyo, wengine waandaa dansi mbadala za kumpinga.

Sherehe ya kuwakaribisha wageni

Sherehe zilianza Alhamisi jioni kwa tamasha la Make America Great Again! (Rejeshea Marekani ukuu wake) katika sanamu ya ukumbusho wa Lincoln mjini Washington DC kama sehemu ya kuwakaribisha wageni.

Waliotumbuiza ni pamoja na wanamuziki wa rock wa 3 Doors Down (pichani juu), ambao wamechomboa albamu mbili zilizokuwa nambari moja kwenye chati Marekani.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mwanamuziki wa muziki wa country Toby Keith pia alitumbuiza. Alitumbuiza pia wakati wa kuapishwa kwa George Bush na Barack Obama.

Haki miliki ya picha Reuters

Mwigizaji mshindi wa tuzo ya Oscar Jon Voight pia alihudhuria tamasha hilo. Ni mmoja wa wasanii wachache waliounga mkono Trump wakati wa kampeni.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mmarekani-mhindi DJ RaviDrums pia alitumbuiza.

Haki miliki ya picha Getty Images

Nyota wa Dreamgirls Jennifer Holliday alitarajiwa kutumbuiza lakini akajitoa baadaye baada ya kushutumiwa sana.

Sherehe rasmi ya kuapishwa kwa Trump

Haki miliki ya picha Getty Images

Heshima ya kuongoza wimbo wa taifa imepewa msichana wa umri wa miaka 16, Jackie Evancho, ambaye alimaliza wa pili katika shindano la America's Got Talent mwaka 2010.

Dansi rasmi

Haki miliki ya picha Getty Images

Sam Moore, wa bendi ya watu wawili ya Sam and Dave, ataongoza wakati wa dansi rasmi ya Liberty and Freedom (Uhuru).

Anasema alishiriki kampeni za kutetea haki za raia na ameshuhudia mabadiliko mengi mazuri katika maiak 81 aliyoishi, lakini anafahamu kwamba lazima watu waungane mikono na kufanya kazi na "rais wetu mpya".

Haki miliki ya picha Getty Images

Radio City Rockettes pia watatumbuiza katika dansi hizo rasmi, ingawa hatua hiyo ilipingwa na baadhi ya wanachama wa bendi hiyo.

Wengine watakaotumbuiza katika dansi hizo ni Tim Rushlow na bendi yake ya Big Band, Silhouettes, Pelican212, The Piano Guys, Circus 1903, Cache Olson, Lexi Walker na Erin Boheme.

Dansi mbadala (za wanaompinga Trump)

Haki miliki ya picha Getty Images

Kutakuwa na dansi mbadala - ambazo zinaitwa Dansi za Amani - ambazo zimeandaliwa na wanaharakati watetezi wa uhuru. Miongoni mwa watakaotumbuiza huko ni dadake Beyonce, Solange Knowles.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mwanamuziki wa jazz mshindi wa tuzo ya Esperanza Spalding pia atatumbuiza katika Dansi ya Amani mjini Washington.

Haki miliki ya picha Getty Images

Bendi ya rock ya Audioslave pia itaandaa tamasha lao la kwanza katika miaka 11, ambapo watatumbuiza katika Dansi ya kupinga Kuapishwa (kwa Trump) mjini Los Angeles, California. Imeandaliwa na bendi ya rock na hip-hop ya Prophets of Rage.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa rock na nyimbo za kitamaduni Jackson Browne, ambaye awali alimuunga mkono Bernie Sanders, atatumbuiza pia dansi hiyo ya kumpinga Trump.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii