Gari lililoendeshwa eneo la wapitanjia lawauwa 3 Melbourne

Gari lililoendeshwa kwenye eneo la wapita njia Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wanasema walilizingira gari na kumpiga risasi dereva kwenye mkono wake na kumtia nguvuni

Watu watatu akiwemo mtoto moja mchanga , wamekufa baada ya gari kuwagonga kwa makusudi wapita njia katikati mwa mji wa Melbourne, kwa mujibu wa polisi.

Takriban watu 29 walijeruhiwa miongoni mwao akiwemo mtoto mchanga ambaye kwa sasa yuko katika hali mahututi baada ya gari kugonga kiti chake cha kusukumwa.

Polisi wanasema walilizingira gari na kumpiga risasi dereva kwenye mkono wake na kumtia nguvuni.

Wanasema tukio hilo linahusiana na ugaidi, lakini inaaminiwa kuwa lina uhusiano na tukio la uchomanaji wa visu lililotokea eneo la kusini mashariki mwa Mji wa Melborne mapema Ijumaa.

Gari hilo liliendeshwa ndani ya wapita njia katika duka la Bourke St Mall, ambalo huwas na shughuli nyingi za ununuzi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kiti cha kusukumia watoto kilichoangushwa kilionekana mahali ambapo mtoto mchanga na mwingine wa miaka miwili waliumizwa

Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo aliiambia BBC kuwa aliona wapita njiawakijaribu kulipisha gari hilo ambalo lilipita kwenye njia ya miguu.

"iliwagonga watu wachache pale nje ya ofisi na kwenye ghala na kuwatupa angani, halafu dereva akaendelea kuendesha," alisema shahidi.

"likawagonga wengine zaidi kuelekekea mbele kwenye njia hii ya miguu. Mara ya kwanza sikufahamu ni nini kinachoendelea. Watu walikuwa wanapiga mayowe na kulikuwa na sauti nyingi kila mahali na vumbi likitimuka, nilifikiri jengo limeporomoka."

Haki miliki ya picha ABC NEWS / RAF EPSTEIN
Image caption Madaktari waliwahudumia majeruhi wapatao 20

Polisi wanasema mtu huyo huyo ndiye aliyemshambulia kaka yake mjaira ya asubuhi katika kitongoji cha Melbourne.

Inaaminiwa baadae alimteka nyara mwanamke mmoja ndani ya gari. Aliachiliwa kabla ya dereva kuendelea kati kati mwa mji na kuanza kuwagonga wapita njia.

Polisi wanasema wanamfahamu mtu huyo, na kwamba ana historia ya muda mrefu ya kufanya vitendo vya ghasia kwa familia yake, matatizo ya madawa ya kulevya na ya kiakili.