Mlanguzi "El Chapo" Guzman afikishwa mahakamani New York

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption El Chapo Guzman

Mlanguzi wa madawa ya kulevya raia wa Mexico Joaquin Guzman amekana mashtaka ya ulanguzi wa madawa ya kulevya, utekaji nyara na mauaji kwenye mahakama ya mjini New York.

Bwana Guzman ambaye pia anajulikana kama El Chapo, alisafirishwa kwenda Marekani siku ya Alhamisi baada ya kushindwa kwenye kesi ya kutaka ashtakiwe nchini Mexico.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa Guzman akiwa mkuu wa kundi la Sinaloa, alihusika na usafirishaji wa viwango vikubwa vya madawa ya heroin na cocaine, na madawa mengine ya kulevya kwenda nchini Marekani.

Mawakili wa El Chapo wanasema kuwa hakuongoza kundi la wahalifu.