Takiban watu 36 wanajulikana kufariki kwenye ajali ya treni India

Maafisa wanaendela na shughuli ya uokozi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wanaendela na shughuli ya uokozi

Idadi ya waliofariki kutokana na ajali ya Treni kusini mashariki mwa India imefikia zaidi ya watu watu 30. Watu wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa baada ya Treni hiyo kuacha reli na

kubingiria ilipokuwa safarini kati ya Jagdalpur na Bhubaneswar katika jimbo la Andra Pradesh usiku wa Jumamosi.Maafisa wa uokozi wamesema watu wengi wangali wamekwama ndani

ya mabehewa ya Treni hiyo na wanahofia idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka. Kilichosababisha ajali hiyo bado haijabainika.

Ajali ya Treni hutokea mara kwa mara nchini India kutokana na miundo mbinu duni na kuchakaa kwa reli.

Mwezi Novemba mwaka jana zaidi ya watu 140 walifariki kutokana na ajali nsawa na hii kaskazini mwa jimbo la Uttar Pradesh

Msemaji wa kitaifa wa uchukuzi wa reli Anil Saxena amesema maafisa wa uokozi wanaendeleza juhudi za kuwafikia manusura wa ajali hiyo.