Theresa May kukutana na Trump Ijumaa ijayo

Theresa May
Image caption Theresa May

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May atajadili kuongeza kile alichokiita uhusiano maalumu baina ya Uingereza na Marekani, pale atapokuwa mmoja kati ya viongozi wa kwanza kukutana na Rais Trump Ijumaa ijayo.

Akihojiwa na BBC, alisema anataraji kutapatikana uwezekano wa kuwa na mkataba mpya wa biashara na Marekani, na maswala kuhusu NATO na ugaidi kuwemo kwenye ajenda.

Bibi May alisema mataifa yote mawili yanakabili changamoto hizo na yanaona vitisho.

Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Bwana Trump siku za nyuma kuhusu wanawake, alisema, hataogopa kumwambia Bwana Trump akiona kuna kitu kisichokubalika.