Israel kujenga nyumba 560 kwa walowezi mashariki mwa Jerusalem

Israil kujenga nyumba 560 kwa walowezi mashariki mwa Jerusalem. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Israil kujenga nyumba 560 kwa walowezi mashariki mwa Jerusalem.

Wakuu wa Israel wameidhinisha ujenzi wa nyumba 560 kwa ajili ya walowezi, mashariki mwa Jerusalem.

Naibu wa meya wa Jerusalem Meir Turjeman, alisema idhini hiyo ilichechelewa kufuatia ombi la waziri mkuu, Benjamin Netanyahu, baada ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilopinga ujenzi wa makaazi hayo.

Marekani haikupinga azimio hilo kwa kura yake ya turufu.

Wapalestina wanatumai kuwa Jerusalem Mashariki itakuwa mji mkuu wa taifa lao litakapoundwa siku za mbele.