Kimbunga Marekani: Watu 18 wauawa Georgia na Mississippi

Mississippi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu wanne wameuawa na kimbunga kusini mwa Mississippi

Watu zaidi ya 18 wamefariki kutokana na kimbunga kikali na hali mbaya ya hewa kusini mwa Marekani, maafisa wa uokoaji wamesema.

Watu wengi wamejeruhiwa. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni majimbo ya Georgia na Mississippi.

Gavana wa Nathan Deal ametangaza hali ya tahadhari katika wilaya saba kusini na katikati mwa Georgia ambapo watu 14 wamefariki.

Watu wanne waliuawa na vimbunga Mississippi siku ya Jumamosi.

Bado kuna hatari ya kimbunga kupiga maeneo ya kusini mwa Florida, idara ya taifa ya hali ya hewa imeonya.

Idara ya huduma za dharura ya Georgia imesema watu 14 walifariki katika wilaya za Cook, Brooks, Dougherty na Berrien katika jimbo la Georgia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maeneo ya Adel, Georgia, yaliathiriwa sana na kimbunga

Nyumba nyingi zimebomolewa katika wilaya ya Cook.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amewasiliana na Gavana Deal na kumpa salamu za rambirambi kutokana na vifo vilivyotokea.

Kusini mwa Mississippi, watu wanne walifariki kutokana na kimbunga ambacho kilikuwa na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi ya 218 km/h (136 mph).

Watu zaidi 50 walijeruhiwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption The violent storms have also damaged property

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii