Erdogan ziarani Tanzania

Ajenda kuu ya ziara ya Erdogan Tanzania itakuwa ni suala la usalama Haki miliki ya picha AFP/getty
Image caption Ajenda kuu ya ziara ya Erdogan Tanzania itakuwa ni suala la usalama

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi barani Afrika ambayo pia itampeleka nchini Musumbiji na Madagascar.

Licha ya rais huyo wa Utukia kufika Tanzania kutafuta mapatano ya kibiashara na mwenyeji John Magufuli, ajenda kuu itakuwa suala la usalama.

Siku za nyuma utawala nchini Uturuki umekuwa ukitaka mataifa ya Afrika kutwaa shule zilizo na uhusiano na muhubiri wa kiislamu Fethullah Gulen mabaye analaumiwa na Uturuki kwa kupanga mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwaka uliopita.

Nchini Tanzanaio shule 11 chini ya mfumo unaojulikana kama Feza, unaosimamiwa na bwana Gulen, zina jumla ya wanafunzi 3000 wengi wao wakiwa ni waislamu.

Uturuki inalaumu shule hizo kwa kukuza wanamgambo kwa vuguvugu lake, ambalo serili inaliona kuwa mpinzani mkubwa.

Kiongozi huyo wa Uturuki anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari baadaye leo katika ikulu la Dar es Salam.