Mama Sarah Obama kupewa ulinzi

Mama Sarah Obama Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mama Sarah Obama

Bibi ya aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama, Sarah Obama ataendelea kupewa ulinzi wa serikali, kwa mujibu wa gazeti la Standard la nchini Kenya.

Nyumbani kwa Sarah Obama katika kijiji cha Kogelo kaunti ya Siaya mashariki mwa Kenya, kuliwekwa ua na baadaye chini ya ulinzi wa polisi wakati mjukuu wake alichaguliwa kuwa rais wa 44 wa Marekani.

Wageni wanaoingia nyumbani kwa Sarah watahojiwa katika kituo hicho cha polisi kilicho nje ya boma lake.

Mkuu wa polisi eneo hilo, Joseph Sawe aliliambia gazeti la Standard kuwa watamtembelea Bi Sarah Obama kujua vile anaendelea.

Kijiji cha Kogelo kinaendelea kuwavutia watalii ambao wangependa kuona alikotoka babake Obama, ambaye amemzungumzia katika kitabu chake Dreams From My Father.