Watoto milioni 18.6 walizaliwa China mwaka 2016

Ni watu wachache walio na ndugu nchini China Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ni watu wachache walio na ndugu nchini China

Idadi ya watoto wanaozaliwa nchini China ilikuwa ya juu zaidi tangu mwaka 2000 licha ya kushuka kwa idadi ya wanawake waliofikisha umri wa kuzaa, kwa mujibu wa maafisa nchini humo.

Kuongezeka huku kumetokana na china kuondoa sheria zake za mtoto mmoja mwaka mmoja uliopita.

Watoto milioni 18.6 walizaliwa mwaka 2016 ambalo ni ongezekeo la asilimia 11.5 kutoka mwaka 2015.

Zaidi ya asilimia 45 ya watoto waliozaliwa mwaka 2016 walikuwa na ndugu mmoja au wawili wakubwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu walio mashambani wakati mwingine waliruhusiwa kuzaa watoto wawili

Maafisa wanasema kuwa ifikapo mwaka 2020 kati ya watoto milioni 17 na 20 wanatarajiwa kuzaliwa nchini China kila mwaka.

Wanakadiria kuwa ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na zaidi ya watu milioni 30 zaidi watakaofanya kazi nchini China.

Sheria za kuzaa mtoto mmoja nchini China zilianza kutumika mwaka 1979 na zinaripotiwa kuchangia China kupoteza watu milioni 5 kila mwaka hali ambayo itashuhudiwa miaka kadha inayokuja

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu nchini china wanazeeka kwa haraka