Askofu aapishwa kuwa mkuu wa tume ya rushwa Kenya

Askofu Wabukala anatajaria kufaulu panye wengi wameshindwa
Image caption Askofu Wabukala anatajaria kufaulu panye wengi wameshindwa

Mkuu mpya wa tume ya kupambana na rushwa nchini Kenya ameapishwa rasmi mjini Nairobi.

Askofu Eliud Wabukala ambaye alikuwa mkuu wa kanisa la kianglikana, alisema anachukua wajibu huo wakati ufisadi unaonekana kukithiri nchini Kenya.

Pia alisema kuwa atahitaji ushirikiano wa mashirika mengine ya serikali kusiaia katika jitidsja za kuamana na ufoisadi. Amenya kwua watu ni alzima wacha kuiba pesa "kuanzia leo".

Mkuu wa sheria nchini Kenya Githu Muigai alimpongeza bwana Wabukala akisema kuwa hakuna mikono bora wa kupigana na vita hivyo ila mikono ya Mungu.

Jitihada za wakuu wa awali wa tume ya kupambana na rushwa zilitatizwa baada ya wao wenyewe kulaumiwa kwa kuhusika kwenye ufisadi.