Pesa za ebola zatoweka Sierra Leone

Malipo ya kufanya kazi mazingira hatari hayakulipwa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Malipo ya kufanya kazi mazingira hatari hayakulipwa

Karibu miaka mitatu baada ya Sierra Leone kukumbwa na ugonjwa wa Ebola mamilioni ya dola zilizokuwa zimechangishwa kupambana na homa hiyo hazijulikani zilipo.

Ukaguzi wa hesabu wa miezi sita ya kwanza kuhusu ugonjwa huo ulionyesha kuwa takriban dola milioni 14 zimetumika vibaya au hazijulikani zilipo.

Ukaguzi huo wa hesabu ulisema kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwepo malipo ya kufanya kazi katika mazingira hatari ya hadi doka milioni 4.

Wakati wa mlipuko wa ebola, lilikuwa jambo la kawaida kuwa malipo hayo yangecheleweshwa.

Hii ilisababisha kufanyika mgomo mwishoni mwa mwaka 2014 katika hospitali ya Kenema.

Makundi ya kuzika maiti yalitoa maiti kutoka viumba vya kuhifadhi na kuziweka kwenye milango ya hospitali wakitaka wapewe marupu rupu yao.