Syria: Mazungumzo ya kutafuta amani yaingia siku ya pili

Astana, Kazakhstan (23 January 2017) Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bashar Jaafari amesema serikali imetoa ujumbe "mzuri na wa matumaini"

Mazungumzo ya amani yanaendelea kwa siku ya pili Kazakhstan kati ya serikali ya Syria na makundi ya waasi.

Majadiliano ya hapo jana jumatatu yaligubikwa kwa malumbano kutoka pande zote.

Kiongozi wa upinzani Mohammad Alloush ameitaja serikali ya Bashar al-Assad kama utawala wa kigaidi.

Serikali kwa upande wake umesema matamshi yake ni matusi na ya uchochezi.

Mazungumzo hayo yalioidhinishwa na Urusi Uturuki na Iran ni ya kwanza ambapo makamanda wa waasi wamekaa meza moja na ujumbe wa serikali pasi kuondoka katikati ya mazungumzo.

Lakini kumekuwa pia na mazungumzo yasio ya moja kwa moja kupitia wawakilishi yaliyolenga namna wanavyoweza kuimarisha makubaliano hafifu ya kusitisha mapigano.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wawakilishi wa makundi makuu ya kigaidi wanashiriki

Kumekuwa na majadiliano pia kuhusu namna ya kuidhinisha mfumo wa uangalizi, na mpango huo utajumuisha wafadhili wakuu wa mazungumzo haya.

Mazuyngumzo haya ya amani yanadhihirisha kukwea kwa Urusi kama mhusika mkuu katika mzozo mkubwa wa Syria.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mohammed Alloush (kati) amesema waasi ni "watu wa amani" the rebels were "men of peace, and at the same time knights of war"

Katika mwaka uliopita, jeshi lake la nguvu lilifanikisha ushindi upande wa rais Assad, na sasa taifa hilo linajaribu kuchukua usukani katika kuielekeza Syria katika amani , lakini bado kuna vikwazo vikubwa.

Mada zinazohusiana