Dikteta wa zamani wa Panama kufanyiwa upasuaji

Manuel Noriega Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dikteta wa zamani wa Panama Manuel Noriega kwenye picha iliyopigwa 2011

Kiongozi wa zamani wa kiimla wa Panama Manuel Noriega ambaye amekuwa gerezani, ameruhusiwa kutumiwa kifungo wa nyumbani ndipo afanyiwe upasuaji kwenye ubongo wake, wakili wake amesema.

Noriega, 82, ambaye awali alikuwa rafiki mkuu wa Marekani, alitawala Panama kuanzia 1983 hadi 1989 alipotolewa kwa nguvu na majeshi ya Marekani.

Anahitaji kutolewa uvimbe kwenye ubongo.

Wakili wake Ezra Angel alifanikiwa kushawishi mahakama kwamba kiongozi huyo wa zamani anafaa kuruhusiwa kujiandaa na pia kupumzika nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji badala ya kukaa hospitali au gerezani.

Noriega alifungwa jela Panama kwa makosa ya mauaji, ulaji rushwa na uporaji wa mali ya umma.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manuel Noriega, kwa sasa ana umri wa miaka 83. Hapa anaonekana akihutubu mwaka 1988

Alihukumiwa akiwa hayupo kortini kwa makosa yaliyotekelezwa wakati wa utawala wake.

Alihamishwa kutoka Ufaransa kwenda Panama kutumikia kifungo chake mwaka 2011.

Atarejeshwa gerezani baada yake kupata nafuu.

Mada zinazohusiana