Polisi wakamata ngozi 5000 za punda Afrika Kusini

Ngozi hiyo hutumika kuongeza urembo na kupunguza kasi ya mwanamke kukoma kujifungua nchini China. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ngozi hiyo hutumika kuongeza urembo na kupunguza kasi ya mwanamke kukoma kujifungua nchini China.

Kampuni ya Afrika Kusini ya kulinda mifugo Farm Animal Protection imefichua maficho mengine ambapo punda huuwawa baada ya maelfu ya ngozi za punda kupatikana.

Inaaminika kuwa wanyama hao walichinjwa kinyume na sheria na kusafirishwa hadi China na kundi moja.

Kulingana na mwanahabari wa BBC Nomsa Maseko ufichuzi huo unajiri kufuatia habari kutoka kwa mwanamke mmoja ambaye alilalamikia harufu mbaya ya nyama iliooza katika shamba moja huko Benoni mashariki mwa mji wa Johannesburg.

Baada ya uchunguzi, zaidi ya ngozi elfu tano za punda zilipatikana katika kasha moja.

Polisi wanasema kashfa hiyo inaongozwa na raia wa China.

Biashara ya ngozi za punda ina thamani ya mamilioni ya dola.

Kulingana na shirika linalokabiliana na ukatili wa wanyama, mahitaji ya ngozi ya punda yameongezeka katika kipindi cha miaka miwili kutokana na mahitaji ya ya juu kutoka China.

Ngozi hiyo hutumika kuongeza urembo na kupunguza kasi ya mwanamke kukoma kujifungua.

Hakuna mtu aliyekamatwa kutokana na ugunduzi huo lakini polisi wanasema kuwa wizi wa punda ,uchinjaji na uuzaji wa ngozi yake umeongezeka nchini Afrika kusini tangu 2015.