Tuzo za Oscar: Filamu ya La La Land yateuliwa mara 14

La La Land pia imeorodheshwa miongoni mwa filamu tisa zinazowania tuzo la filamu yenye picha bora. Haki miliki ya picha LIONSGATE
Image caption La La Land pia imeorodheshwa miongoni mwa filamu tisa zinazowania tuzo la filamu yenye picha bora.

Filamu ya muziki ya La La Land ni miongoni mwa filamu zilizoteuliwa ambazo huenda zikashinda mataji katika tuzo za Oscar baada ya kuteuliwa mara 14

Ryana Gosling na Emma Stone wameteuliwa kuwania mwigizaji bora wa kiume na wa kike kwa majukumu yao katika filamu hiyo ya mapenzi.

Filamu hiyo pia imeorodheshwa miongoni mwa filamu tisa zinazowania tuzo la filamu yenye picha bora.

Filamu ya Sci-fi, Arrival na Moolight pia zimeorodheshwa mara nane kila moja.

Mwigizaji anayeigiza kama Bi Moneypenny katika filamu ya James Bond ,amesema kuwa kuwa anafuraha isio na kifani kwa kuteuliwa.

Uteuzi wa mwaka huu umeangazia rangi huku wagombea 7 kati ya 20 wanaowania taji la uigizaji bora wakitoka miongoni mwa makabila ya wachache.

Waigizaji ni pamoja na Denzel Washington, aliyeteuliwa kuwania taji la mwigizaji bora katika filamu ya ''Fences'' na Ruth Negga kwa jukumu lake katika filamu ya ''Loving''.

Kwa kipindi cha miaka miwili iliopita wagombea wote walioteuliwa wamekuwa watu weupe.

Meryl Streep ameteuliwa kwa mara ya 20 kwa jukumu lake katika filamu ya Florence Foster Jenkins.