Ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama

Ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama Haki miliki ya picha Adam Elliott
Image caption Ashtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama

Mtu mrefu ameshtakiwa kwa kuendesha gari akiwa amesimama baada ya kukiri kupeleka gari vibaya.

Adam Elliott alituhumiwa kwa kuwaonyesha madereva wengine kichwa chake kikiwa kinaonekana juu ya paa la gari hilo aina ya Ford Ka.

Elliott mwenye umri wa miaka 26 kutoka mji wa Newcastle, ambaye ana urefu wa mita mbili alikiri kufanya makosa hayo katika mahakama ya Newcastle lakini akalaumu urefu wake.

Haki miliki ya picha Adam Elliott
Image caption Adam Elliott

Akizungumza baada ya kesi hiyo, alisema: Sikuwa nimesimama, mimi ni mrefu ndio maana.

Jaji Robert Adams alisema kuwa ni wazi kwamba Adam alitaka kuonekana akiendesha gari akiwa amesimama ili kuonyesha urefu wake.

''Ilikuwa kitu hatari sana kufanya'',alisema.