Ivory Coast yavuliwa ubingwa Afcon

Moroco Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Moroco wakishangilia

Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la mataifa ya afrika tembo wa Africa Ivory Coast, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu baada ya kuchapwa kwa bao 1-0 na Simba wa Atlas Moroco

Goli pekee liliowaondoa miamba hao wa soka wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo.

Nayo timu ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo ilitambia Togo kwa kuichapa kwa mabao 3-1 na hivyo kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara kwa kundi C kwa alama 7 huku Moroco wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Moroco na Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo wanafuzu katika kundi hilo la huku Ivory Coast na Togo zikitupwa nje ya michuano hiyo.