Al-Shabab washambulia hoteli Mogadishu

Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wanachama wa al-Shabab wameshambulia hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Haki miliki ya picha EPA

Watu hao wenye silaha waliingia kwenye hoteli hiyo baada ya kulipuliwa kwa mabomu mawili kwenye lango la kuingia kwenye hoteli hiyo ya Dayah.

Waziri wa usalama Abdirizak Omar Mohamed amesema watu 10 waliuawa na wengine 50 kujeruhiwa.

Miongoni mwa waliokuwa wakiishi kwenye hoteli hiyo, ni wabunge waliochaguliwa majuzi katika bunge la Somalia.

Kundi la al-Shabab limekiri kuhusika.

Walioshuhudia wanasema washambuliaji walitumia gari lililokuwa limetegwa vilipuzi kulipua lango na kuingia ndani ya hoteli na kisha wakaanza kuwafyatulia watu risasi.

Muda mfupi baada ya mlipuko wa kwanza, gari jingine lililipuka na kuua watu waliokuwa wamekusanyika eneo hilo kufuatia mlipuko wa kwanza. Wengine wengi walijeruhiwa.

Manusura wamesimulia jinsi wageni waliokuwa hotelini walivyojificha mvunguni mwa vitanda vyao na wengine kuruka nje kupitia madirisha kukwepa washambuliaji.

Hassan Nur ameambia AP: "Washambuliaji walifungua milango kwa nguvu na wakati mmoja walijifanya maafisa wa uokoaji na kuwaambia waliokuwa ndani kwenye vyumba watoke nje kisha wakawafyatulia risasi."

Afisa wa polisi Kanali Abdiqadir Hussein tameambia Reuters kwa maafisa wa polisi walifanikiwa kuingia kwenye hoteli hiyo na kuwaua wavamizi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la al-Shabab limekiri kuhusika

"Tumewaokoa watu na kuhitimisha operesheni hiyo kwenye hoteli ya Dayah," amesema.

Hoteli hiyo inapatikana chini ya maili moja kutoka kwa ikulu ya rais na ni maarufu sana kwa wageni waheshimiwa.

Shambulio hilo limetekelezwa wakati ambapo taifa hilo linajiandaa kwa uchaguzi wa rais usio wa moja kwa moja, ambapo wabunge ndio watakaomchagua rais.The attack comes at a time when the country is preparing for indirect elections where MPs are set to choose a president.

Mada zinazohusiana