Mwana wa Michael Jackson asema babake aliuawa

Paris Jackson na marehemu babake Michael Jackson Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paris Jackson na marehemu babake Michael Jackson

Mwana wa kike wa pekee wa nyota wa muziki wa Pop marehemu Michael Jackson , Paris amesema kuwa anaamini kwamba babake aliuawa.

Katika mahojiano yake ya kwanza, Paris aliambia Rolling Stones ana hakika kwamba kifo cha babake mwaka 2009 kilipangwa.

Mwanamuziki huyo alifariki baada ya madai kwamba alikula dawa nyingi ya kupunguza maumivu.

Daktari wake Conrad Murray baadaye alipatikana na hatia ya mauaji ya kutokusudia.

Lakini mwanawe Paris anaamini kuna taarifa zaidi kuhusu habari hiyo.

Alisema kuwa mara nyengine alituambia kwamba kuna watu wanamfuata kumkamata, alisema.

Na mara nyngine alisema: 'Wataniuwa siku moja'. Alipoulizwa na Brian Hiatt iwapo anadhani babake aliuawa ,kijana huyo wa mika 18 hakusita kusema 'ndio' .

Aliendelea kusema: Watu wengi walitaka babake auawawe na kwamba alikuwa anajaribu kuwashtaki.

Kijana huyo hatahivyo hakutaja watu fulani na hakumshirikisha Conrad Murray katika tuhuma zake.