Serikali yamnyonga mwanamfalme Kuwait

Serikali ya Kuwait imewanyonga wafungwa saba kwa mara ya kwanza tangu 2013 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali ya Kuwait imewanyonga wafungwa saba kwa mara ya kwanza tangu 2013

Serikali ya Kuwait imewanyonga wafungwa saba kwa mara ya kwanza tangu 2013, akiwemo mmoja wa jamaa ya familia ya kifalme.

Walinyongwa katika jela ya Central kulingana na taarifa iliotolewa na kitengo cha habari cha serikali Kuna.

Jamaa huyo kutoka familia ya kifalme alitajwa kuwa Faisal Abudallah Al Jaber Al Sabah ambaye alipatikana na hatia ya kupanga mauaji mbali na kumiliki silaha kinyume na sheria.

Wafungwa wengine walionyongwa ni pamoja na raia wa Ufilipino, Misri, Ethiopia na Bangladesh.

Walipatikana na hatia ya uhalifu ikiwemo mauaji, jaribio la mauaji ,utekaji nyara na ubakaji.

Mwanamfalme aliyekiri kuua akatwa shingo Saudia

Al Sabah alipatikana na hatia ya kumuua mwanamfalme mwengine mwaka 2010.

Mwandishi wa BBC mashariki ya kati ambaye ni muhariri wa eneo hilo Sebastian Usher alisema kuwa si jambo la kawaida kwa jamaa wa familia ya kifalme katika eneo la Ghuba kupelekwa jela ama hata kunyongwa.

''Kesi hizo huthibitisha kwamba hakuna mti asiyeweza kushtakiwa'',aliongezea.

Miongoni mwa wale walionyongwa ni Nusra al_Enezi, raia wa Kuwait ambaye alipatikana na hatia ya kuchoma moto hema wakati wa harusi ya mumewe ambaye alikuwa anaoa mke wa pili.

Moto huo uliwaua takriban watu 50.