Benghazi yaokolewa toka kwa wapiganaji, Libya

Wapiganaji Libya Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wapiganaji Libya

Wapiganaji wenye itikadi kali nchini Libya wamepoteza ngome yao ya mwisho, katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Benghazi.

Wapiganaji wanaomtii kiongozi wa kijeshi, Jemedari mkuu Khalifa Hefter wamesema wamewaondoa wanamgambo wa kiislamu katika wilaya ya Ganfouda.

Eneo hilo lilikuwa limezingirwa kwa miezi kadhaa na limeonekana kuwa na mapigano mabaya zaidi katika kuidhibiti Benghazi.

Baadhi ya wapiganaji wa kiislamu wana mafungamano na mtandao wa Al Qaeda.

Jemedari mkuu Hefter aliongoza mapambano dhidi yao, ingawa jeshi lake halitambuliwi na serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.