Uhamiaji Marekani: Mameya wampinga Donald Trump

Donald Trump awataka mameya kutiia mkazo sheria za uhamiaji
Image caption Donald Trump awataka mameya kutiia mkazo sheria za uhamiaji

Mameya wa miji mingi nchini Marekani wanaowahifadhi wahamiaji haramu wamesema kuwa hawatatishwa na mpango wa rais Donad Trump kupunguza ufadhili wa kieneo iwapo hawatashirikiana naye katika mpango wake wa kutilia mkazo sheria za uhamiaji.

Meya wa mji wa New York Bill de Blasio amesema kuwa ataupinga mpango huo wa rais na kwamba ana ushahidi wa kutosha wa kisheria.

Meya wa Boston Marty Walsh amesema kuwa agizo hilo linawalenga moja kwa moja raia wa Boston na maadili yao na kuongezea kwamba atawahifadhi wahamiaji ndani ya ukumbi wa mji iwapo inawezekana.

Meya wa mji wa Seattle Ed Murray amesema kuwa mji wake hautashurutishwa na amewaagiza maafisa wake kuangazia bajeti yao upya ili kukabiliana na hatari yoyote ya kupunguziwa ufadhili.