Adama Barrow ataka wanajeshi wa Magharibi kusalia Gambia

Wanajeshi wa Senegal wanalinda ikulu ya Gambia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Senegal wanalinda ikulu ya Gambia

Rais mpya wa Gambia amevitaka vikosi vya mataifa ya Magharibi mwa Afrika kusalia nchini humo kwa miezi sita , kulingana na chombo cha habari cha AFP ambacho kimenukuu maafisa wa Umoja wa Mataifa.

Adama Barrow anatarajiwa kurudi nyumbani ili kuchukua mamlaka.

Viongozi wa mataifa ya magharibi walituma wanajeshi nchini Gambia wiki iliopita ili kumshinikiza aliyekuwa rais wa taifa hilo yahya Jammeh kuwachia mamlaka baada ya kushindwa katika uchaguzi mnamo mwezi Disemba.

Mohammed Ibn Chambas ,afisa mwandamizi katika eneo la Magharibi mwa Afrika ,alitoa matamshi hayo katika mkutano na wanahabari nchini Senegal, kwa mujibu wa AFP.

Rais wa Gambia ametaka vikosi hivyo kusalia kwa miezi sita zaidi, na sasa ni ECOWAS kuamua.