Wachimba mgodi 14 wakwama ndani ya ardhi Tanzania

Wachimba mgodi 14 wamekwama ndani ya mgodi baada ya kuporomoka eneo lililo kaskazini magharibi mwa Tanzania. Haki miliki ya picha Justin Purefoot
Image caption Wachimba mgodi 14 wamekwama ndani ya mgodi baada ya kuporomoka eneo lililo kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Wachimba mgodi 14 wamekwama ndani ya mgodi baada ya kuporomoka eneo lililo kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Wafanya kazi hao wakiwemo raia mmoja wa China na 13 wa Tanzania, walifukiwa na udongo umbali ya mita 38 chini ya ardhi katika eneo linalomilikiwa na kampuni ya Kichina.

Kulinga na kituo cha runinga cha ITV jitihada za uokoaji zinaendelea.

Kamishina wa eneo la Geita Ezekiel Kyunga, ambaye yuko eneo hilo aliiambia runinga ya taifa kuwa anaamini wataokolewa wakiwa hai.

Mwezi Machi mwaka uliopita, wachimba mgodi watano sehemu tofauti ya eneo hilo, waliaga dunia baada wa kukwama chini ya ardhi wakitafuta dhahabu.