Kilimanjaro Warrios kuingia kambini jumapili

Tanzania Haki miliki ya picha Google
Image caption Kikosi cha timu ya vijana ya Tanzania

Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 'Kilimanjaro Warriors' inatarajiwa kuingia kambini Januari 29, mwaka huu.

Timu hiyo itaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali za Olimipiki zitakazofanyika jijini Tokyo Japan, mwaka 2020.

Kambi hiyo itakua ya wiki moja itafanyika kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na kamati ya olimpiki (TOC) watafanya utaratibu wa timu hiyo kwa kuipatia michezo ya kujipima nguvu ndani na nje ya nchi.